Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman Ali maarufu ‘Morocco’, kuelekea mchezo wa robo fainali ya michuano ya CHAN 2024 kati ya Tanzania na timu ya Taifa ya Morocco, amewaomba watanzania wasimuite jina lake la utani la Morocco hadi mchezo huo utakaomalizika siku ya Ijumaa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Hemed ameyasema katika mahojiano na TBC, mbashara kutoka Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.
Amesisitiza kuwa Stars wapo imara na tayari kukabiliana na Morocco, huku akionyesha matumaini ya kikosi chake kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya CHAN