NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO
Akizungumza leo (Agosti 19, 2025) katika hafla ya utiaji saini uliofanyika katika Ofisi za ADEM, Bagamoyo, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Innocent Mgeta, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, alisema mpango huo utahusisha mafunzo ya wakuu wa shule ana kwa ana na kupitia moduli za mtandaoni.
Aidha amesema kuwa mpango huu unalenga kufikia shule zote za sekondari ukihusisha wakuu wa shule takribani 6,000 katika Tanzania Bara na visiwani (Zanzibar).
Kupitia ushirikiano huu, wakuu wa shule za Sekondari na maafisa elimu wa Halmashauri Idara ya Elimu Sekondari watapatiwa mafunzo kuhusu uongozi nausimamizi wa elimu utakaowawezesha kuboresha usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule za Sekondari nchini.

