Wadau wamekuwa na maswali mengi kwanini mshambuliaji wa Simba sc Jonathan Sowah atakosa mchezo wa ufunguzi wa NBCPL dhidi ya watani zao Yanga sc, ufafanuzi huu hapa.
Kwa nini Sowah hachezi derby (Ngao ya Jamii)? Ana adhabu ya kadi nyekundu aliyooneshwa akiwa na Singida Black Stars Vs Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.
Kwa nini apewe kadi Singida BS then pamoja na kuhama aje kuitumikia akiwa Simba? Kadi anaadhibiwa mchezaji sio timu unahama nayo.
Mbona mashindano tofauti? Mashindano yote ya ndani yako chini ya TFF kuanzia Ligi Kuu, CRDB Bank Federation Cup hadi Ngao ya Jamii. Kanuni ni zile zile zinagusa pande zote.
Mfano Simba ingekuwa imechukua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika 2024/25 kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya 2025/26 mashindano ya CAF, CAF Super Cup, bingwa wa Shirikisho (CAFCC) dhidi ya bingwa wa Ligi ya Mabingwa (CAFCL),
Yusuf Kagoma asingecheza huo mchezo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoadhibiwa mechi ya fainali Vs RS Berkane.