Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limetangaza kuwa mashabiki wanaokaa eneo la mzunguko siku ya kesho wafike kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa na watapewa tiketi ambazo zimenunuliwa na wadau kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo.
Mashabiki hao ambao watahitaji kupata tiketi hizo watakiwa kufika katika geti A upande wa chuo cha DUCE na geti B upande wa Uhasibu.
“Tupo robo fainali tunakwenda nusu fainali pamoja, njoo Benjamin Mkapa kesho suala la kuingia uwanjani tuachie sisi tayari tumelimaliza kwa wenetu wa Mzunguko, mageti yetu ni A upande wa DUCE na B upande wa Uhasibu”.