Baadhi ya watumishi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wakijadili mara baada ya kugundua mteja wao wa mtaa wa uhuru akiwa amejiunganishia umeme kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali
Fundi wa shirika la umeme (TANESCO)mkoa wa Mwanza, Kilion Olang akitoa mita ya umeme ya mteja ambaye amejiunganishia umeme kinyume na taratibu na kupelekea hasara kwenye shirika hilo
Afisa huduma kwa wateja wa shirika la umeme (TANESCO)Frank Mbayo akizungumza na Fullshangwe mara baada ya kukagua mita ya mteja wao na kubaini amechepusha umeme na kupelekea hasara kwenye shirika hilo.
Msimamizi Idara ya kudhibiti Mapato Tanesco mkoa wa Mwanza, Chuzye Peter amewataka wananchi (wateja wao) kujiepushana na mafundi wa mtaani ambao wanafanya kazi kinyume na sheria
…………….
Na Hellen Mtereko,
Mwanza
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Mwanza limemkamata Felister Binza aliyejiunganishia umeme kinyemela kwenye chumba chake cha biashara kilichopo dampo mtaa wa uhuru.
Binza ambae ni mfanyabiashara wa nguo katika mtaa wa Uhuru wilaya ya Nyamagana Mkoani hapa alikamatwa jana baada ya kufanyika msako wa kushitukiza ndipo akakutwa akiwa amechepusha umeme kutoka kwenye nguzo na kuingiza kwenye chumba cha duka lake.
Ikumbukwe kwamba TANESCO wako kwenye oparesheni maalumu ya kuwasaka na kuwachukulia hatua kali watu wote wanaojihusisha na uharibifu wa miundombinu ya umeme pamoja na wizi wa nishati hiyo.
Aidha, Binza alivyoulizwa kwanini anajiunganishia umeme kinyemela alijibu yeye hajui chochote kwani ni mpangaji hivyo akasema aulizwe mmliki wanyumba hiyo.
Naye Afisa huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Mwanza, Frank Mboya alisema kuwa tukio hilo linasababisha hasara kwenye Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na ni kinyume cha sheria hivyo anayebainika kufanya hivyo anaweza kufungwa au kutoa faini ama kukabiliana na adhabu zote.
Alitoa wito kwa wananchi kufuata taratibu zinazotakiwa kwani kila sehemu wapo watumishi wa TANESCO ambapo mtu ambaye anahitaji huduma ya kuunganishiwa umeme anapaswa kwenda ofisini ili aweze kukutana na uongozi na kupatiwa huduma hiyo na kufanyiwa kazi hiyo kwa haraka bila ya usumbufu wowote.
“Huduma zetu ni za haraka hakuna janja janja yoyote ile hivyo wananchi wafuate utaratibu na siyo kujiunganushia umeme kinyume na tararibu zilizowekwa na Serikali, “alisema Mboya.
Kwa upande wake Msimamizi wa Idara ya Kudhibiti Mapato (TANESCO) Mkoa wa Mwanza, Chuzye Peter alisema hujuma hiyo imefanywa kZach kuchepusha umeme hivyo kufanya tokeni za umeme kutohesabiwa.
Alisema kuwa katika uchunguzi waliofanya wamebaini kuwa mtu huyo alikuwa akitumia umeme ambao hajalipia hivyo amelisababishia shirika hilo hasara kwa muda mrefu.
Hata hivyo amewataka wananchi kujiepusha na mafundi vishoka wanaowaunganishi umeme kinyume na taratibu zilizowekwa kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria endapo ikigundulika hatua kali. Zitachukuliwa.
Fullshangwe Blog ilifanya jitihada za kumtafuta mmiliki wa nyumba kwa njia ya simu akadai hawezi kuzungumza kutokana na kwamba alikuwa msibani.