DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu nchini na DJ maarufu Rommeo Jones, anayefahamika zaidi kama Rommyjons, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuweka wazi kiwango chake cha juu katika sanaa ya uigizaji. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rommyjons ametoa kauli ya kujiamini inayosisitiza kuwa kwa sasa hana mpinzani katika tasnia hiyo.
“Nadhani ni muda wa kuweka vitu sawa sasa! Hakuna anaeniweza kwa kuigiza kwa sasa na hilo linafahamika,” ameandika Rommyjons katika sehemu ya ujumbe wake.
“Licha ya kuwa na muda mfupi katika tasnia ya filamu, Rommyjons amedai tayari ameshachukua tuzo kadhaa zikiwemo za chaguo la watazamaji, jambo analoliona kama uthibitisho wa uwezo wake. “ameendelea kusema:
“Nina muda mchache sana kwenye tasnia ya filamu lakini nishachukua matuzo kibao ikiwemo muigizaji bora tena chaguao la watazamaji. Nisipojisifia hakuna atakayenisifia.”
Rommyjons pia hakusita kuwashukuru mashabiki wake kwa sapoti wanayompa, huku akiwaahidi burudani zaidi kwa mwaka huu:
“Niwashukuru sana mashabiki zangu. Nina series kama tatu zinakuja kabla ya mwaka kuisha, mtafurahi sana,” amehitimisha.
Kauli hiyo imezua mjadala miongoni mwa mashabiki na wapenzi wa filamu, wengi wakisubiri kwa hamu kazi mpya kutoka kwa msanii huyo anayeonekana kuwa na malengo makubwa ndani ya tasnia ya uigizaji.
The post Rommy Jons ajiamini: “Hakuna anaeniweza kuigiza, series mpya zaja” first appeared on SpotiLEO.