DAR ES SALAAM: NEO Maema, kiungo mshambuliaji kutoka Afrika Kusini, jana alitambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa Simba akijiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mkataba wa miaka mitatu.
Maema, aliyehamia Simba kwa uhamisho wa bure kutoka Mamelodi Sundowns, alionesha msisimko mkubwa kuanza maisha mapya nchini Tanzania.
Safari yake ya Soka
Maema mwenye umri wa miaka (30) alianza taaluma yake nchini Afrika Kusini akiwa na Bloemfontein Celtic, kisha kuhamia Mamelodi Sundowns mnamo 2021, ambapo alicheza zaidi ya mechi 120, akifunga magoli 13 na kutoa pasi za goli 14.
Katika kipindi chake Sundowns, alishinda mataji manne ya ligi, Nedbank Cup, MTN8, na taji la African Football League.
Pia, Maema amecheza na timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, akiwa nahodha katika mashindano ya CHAN 2024.
Ujio wa Maema unalenga kuimarisha safu ya ushambuliaji na kuongeza ubora ndani ya kikosi cha kocha Fadlu Davids, ambaye pia ni raia wa Afrika Kusini.
Mashabiki wa Simba wamepokea ujio wa mchezaji huyo kwa shangwe, wakiamini uzoefu na kipaji chake vitasaidia timu kushindana kwenye ligi na mashindano ya kimataifa, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika
The post Mjue Maema, kiungo mshambuliaji wa Simba first appeared on SpotiLEO.