
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeondolewa kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa robo fainali uliochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 65 kupitia kwa Lamlioui, na kuipa Morocco tiketi ya kutinga nusu fainali.
Kwa matokeo hayo, Tanzania inaungana na Kenya kutupwa nje ya michuano hiyo. Kenya walifungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Madagascar katika robo fainali nyingine.
Hivyo, Morocco imeungana na Madagascar kwenye hatua ya nusu fainali huku ikisubiri washindi wa michezo mingine ya robo fainali.
Matokeo ya Robo Fainali (CHAN 2024):
Tanzania 0-1
Morocco
Kenya 3(3)-3(4)
Madagascar
Â