
Dodoma, Agosti 22, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtembelea Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dkt. Abdallah Juma Sadala (Mabodi), aliyelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.
Ziara hiyo ililenga kumjulia hali kiongozi huyo wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.