NIGERIA: MWANAMUZIKI wa Nigeria Burna Boy amezungumzia dhana potofu kwamba anakwepa kunyoa makwapa kwa sababu chanzo cha mafanikio yake kinatokana na voodoo.
Hayo yanakuja baada ya mashabiki wake mitandaoni kutofurahishwa na picha ikimuonesha mwanamuziki huyo akiwa na nywele nyingi kwenye makwapa.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Apple Music, nyota huyo aliyeshinda Grammy alidai kwamba madai hayo ni vichekesho tu hayana maana yoyote.
Mhojiwa aliuliza: “Unaweza kusema ni maoni gani potofu ya kawaida kuhusu Burna Boy?”
Burna Boy alijibu hivi: “Moja ni kwamba sipendi kunyoa makwapa.” Watu hufikiri kwamba ni kama Samsoni katika Biblia ambaye ana nguvu zake kutokana na nywele zake.
“Kuna baadhi ya watu wanaodai kwamba kwapa langu ndipo nguvu zangu ziko kwa sababu sinyoi. Nchini Nigeria unasikia mambo ya kichaa. Kuna baadhi ya watu wanafikiri hiyo ni voodoo, kana kwamba nguvu zangu ziko kwapani.
Sijui hata jinsi ya kuielezea. Ni upuuzi tu ambao unaendelea hakuna chochote cha maana.
The post Burna Boy aweka wazi sababu ya kutonyoa makwapani first appeared on SpotiLEO.