NIGERIA: MWANAMUZIKI wa Afrobeat ambaye ni mjukuu wa nguli Fela Kuti, Made Kuti, amejibu shutuma mbaya kuhusu ndoa yake na mke wake Inedoye Onyenso.
Fela Kuti alifunga pingu za maisha na Inedoye Onyenso kwenye sherehe ya harusi ya kiserikali huko Lagos mnamo Novemba 2023.
Ndoa yao imekuwa ikikosolewa na vigogo waliowashutumu kwa kuchanganya damu kutokana na asili zao tofauti za kikabila.
Akijibu chapisho la X la, @AdemolaOgudu, aliyemwita “mwanamme mjinga wa Kiyoruba kwa kuoa mwanamke wa Igbo, Kuti alijibu kwa kuanza kwa kushangaa kukosolewa kuoa kisa tofauti ya makabila yao: “Huo ni upungufu wa akili na ni mawazo ya utumwa.”
Aliwataka wakosoaji wa ndoa yake wajielimishe kuhusu historia ya makabila yao iliyoachwa na ‘Pan-Africanists’ aliowataja akiwemi Nyanyake Funmilayo Ransome-Kuti, babu yake Fela Kuti, Kwame Nkrumah, na Thomas Sankara.
Fela amesisistiza kuwa Afrika itapata mambo mengi kama itaungana na kuungana kwenyewe ndiyo kuoana bila kujali tofauti ya makabila yao.
The post Made Kuti: Kwani ni dhambi kumuoa mwanamke wa Kiigbo? first appeared on SpotiLEO.