Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa tamko la kuitimiza ahadi aliyoitoa kabla ya mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Mporocco uliopigwa jana majira ya saa 2:00 usiku kwenye mashindano ya fainali za CHAN 2025 yanayohusu wachezaji wa ndani ambapo Stars ilifanikiwa kuingia Robo fainali lakini jana ikashindwa kupenya kuingia nusu fainali baada ya kutolewa kwa Goli moja dhidi ya timu ya taifa ya morroco.
“Kwa namna alivyodaka, tumpe tu gari yake Toyota Crown. Lengo letu halikutimia, lakin tuendele kujipanga. Hongera sana Taifa Stars, hongera sana Watanzania. Tumethubutu. Tukipigwa kama tumewapiga, na tukiwapiga tumewapiga kabisa” – Amesema Chalamila
Hayo ameyasema baada ya Stars kutolewa na mlinda mlango wa Stars Yakoub Suleiman kuonesha kiwango bora kwa kuchomoa mipira mingi iliyokuwa na hatari kwenye lango la Stars.