MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Juma Mkambala ‘Jux’, na mkewe Priscilla, wamepata baraka ya mtoto wao wa kwanza mtoto wa kiume aliyepewa jina la Rakeem Mkambala.
Taarifa hii njema imethibitishwa na mama mzazi wa Priscilla, ambaye ameeleza furaha ya familia kwa ujio wa mtoto huyo.
Hii inafungua ukurasa mpya kwa familia ya Jux na Priscilla, ambao wamekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii tangu harusi ya kifahari ya JP2025, kutangazwa kwa ujauzito, hadi sherehe ya kufichua jinsia ya mtoto wao.
Kwa mashabiki wa Jux, hii ni hatua kubwa si tu katika maisha yake binafsi, bali pia katika safari yake kama msanii ambaye amekuwa akifuatiliwa kwa karibu. Kuanzia sasa, Jux anavaa kofia mpya baba wa familia, huku Priscilla naye akiingia rasmi katika majukumu ya uzazi kama mama mpya mjini.
Familia hii changa sasa inaanza maisha mapya ya ulezi na malezi, huku mashabiki wakitoa pongezi na kheri njema kwao.
The post “Jux na Priscilla wamkaribisha mtoto wa kwanza – Rakeem Mkambala” first appeared on SpotiLEO.