KILIMANJARO:KIKOSI cha JKT Queens FC kipo kambini mjini Moshi kuendelea na maandalizi ya mashindano ya CECAFA yatakayofanyika nchini Kenya kuanzia Septemba 4 hadi 16, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa JKT Masau Bwire, kambi hiyo inaendelea vizuri ambapo wachezaji wote wameripotiwa kuwa katika hali nzuri kiafya huku morali ikiwa juu, wakilenga kuandika historia nyingine katika mashindano hayo ya kimataifa.
Mashindano ya CECAFA mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha timu tisa kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, huku droo ikitarajiwa kufanyika kesho nchini Kenya.
Kocha na benchi la ufundi la JKT Queens wameweka mkakati kabambe kuhakikisha wachezaji wanakuwa katika kiwango bora kitakachowawezesha kushindana kwa ushindani mkubwa na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka nchini Septemba mosi kuelekea Kenya kwa ajili ya kuanza kampeni zake za CECAFA.
The post JKT Queens kambini Moshi kujiandaa na CECAFA first appeared on SpotiLEO.