Nahodha wa timu yaTaifa ya wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ Opa Clement ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya SD Eibar ya ligi kuu wanawake nchini Hispania.
Opa nahocha wa zamani wa Simba Queens na Besitkas ya Uturuki amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja hadi June 2026 akitokea timu ya FC Juarez ya nchini Mexico.
Opa anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu Hispania.