“Niwe tu muwazi bado Nahitaji Mchezaji mmoja mwenye X Factor kwenye eneo la ushambuluaji, najua tumepata sapoti kubwa Sana kutoka kwa Rais Mo Dewji na mchango wake Msimu huu umekuwa mkubwa Sana”
“Natumai sasa tunapoelekea mwishoni mwa usajili Jayrutty anaweza kutusaidia kumpata Mchezaji huyo mmoja mkubwa ambaye anaweza kutupa utofauti kwenye eneo la mwisho”
“Unakumbuka Baadhi ya mechi ngumu Msimu uliopita tulikuwa tunakosa Mchezaji mkubwa ambaye anaweza kukupa hizo x Factor, mechi kama ya Fainali , mechi dhidi ya Yanga tulikuwa tunakosa Mchezaji kama huyo”
“Na unajua tunahitaji kuwaovertake Yanga ambao unajua ni kwa Kiasi Gani wanakuwa Bora kwenye Mechi kubwa, lakini pia tunakazi kubwa ya kufanya kimataifa” -Fadlu Davs Kocha wa Simba baada ya Mchezo wa Jana aliiambia Azam Tv!