LONDON: MABINGWA wa Kombe la Carabao Newcastle United wataanza kutetea taji hilo kwa kumenyana na timu ya daraja la tatu, Bradford City huku Liverpool washindi wa pili wa msimu uliopita wakiwakaribisha Southampton, Anfield.
Newcastle, ambao ushindi wao dhidi ya Liverpool ulimaliza ukame wa miaka 70 wa makombe ya ndani, hawakuhusika kwenye raundi ya pili pamoja na klabu nyingine za Premier League zilizoshiriki Ligi ya Mabingwa au Europa League.
Manchester City watasafiri kuifuata timu ya League One Huddersfield Town huku Chelsea wakichuana na Lincoln City na Arsenal wakiwa Port Vale. Mechi mbili zitahusisha timu kutoka EPL Brentford dhidi ya Aston Villa na Wolverhampton Wanderers kumenyana na Everton.
Grimsby Town ya daraja la nne, ambayo ilishtua ulimwengu kwenye raundi ya pili kwa kuwaondoa washindi mara sita wa kombe hilo Manchester United jana Jumatano, itavaana na timu ya daraja la pili Sheffield Wednesday.
Droo kamili:
Port Vale v Arsenal
Swansea City v Nottingham Forest
Lincoln City v Chelsea
Tottenham Hotspur v Doncaster Rovers
Brentford v Aston Villa
Huddersfield Town v Manchester City
Liverpool v Southampton
Newcastle Utd v Bradford City
Sheffield Wednesday v Grimsby Town
Wolves v Everton
Crystal Palace v Millwall
Burnley v Cardiff City
The post Raundi ya 4 Carabao cup hii hapa first appeared on SpotiLEO.