NEWCASTLE: KLABU ya Newcastle United inakaribia kuinasa saini ya mshambuliaji wa Stuttgart, Nick Woltemade, katika kile kinachoonekana kama hatua ya kuziba pengo la mshambuliaji wao wa sasa Alexander Isak hatua ambayo inaweza kuwa mwanga wa matumaini katika harakati za Liverpool kumnasa.
Inafahamika kuwa Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, yuko njiani kuelekea Tyneside baada ya makubaliano kufikiwa na baina ya Newcastle na timu hiyo ya Bundesliga.
Woltemade, ambaye pia amekuwa kivutio kwa vigogo Bayern Munich katika dirisha hili la usajili, atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili kukiwasha EPL na UEFA katika dimba la St James’ Park.
Bado hakuna uthibitisho wa ada ya usajili huo, lakini chanzo cha ndani ya klabu kiliidokeza BBC Sport kuwa ada hiyo inaweza kuweka rekodi ya klabu baada ya hapo awali Newcastle kutumia Pauni milioni 63 kumfanya Isak kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia yao miaka mitatu iliyopita alipowasili kutoka Real Sociedad.
Isak, bila shaka bado amedhamiria kujiunga na Liverpool na uhamisho wa Woltemade bado unaweza kuwapa mabingwa hao moyo wa kurejea mezani katika siku za mwisho za dirisha usajili baada ya dau la pauni milioni 110 kukataliwa mwezi uliopita.
Katika taarifa ya wiki iliyopita, Newcastle haikuona masharti ya kumuuza Isak yakitimizwa yaani kupata washambuliaji wawili wenye ubora pamoja na kupokea ofa nono zaidi kutoka Liverpool.
Hata hivyo, Magpies wamefikia makubaliano na Woltemade, ambaye anacheza kama mshambuliaji wa kati anayeweza kuongoza safu hiyo kwa sasa, na pia mchezaji mdogo mwenye uwezo na nafasi kubwa ya kuimarika zaidi, ambayo ni kama hatua ya kwanza muhimu.
Woltemade hakuwa chaguo la kwanza alipowasilli Stuttgart kwa uhamisho wa bure kutoka Werder Bremen msimu uliopita. Lakini mshambuliaji huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6 alifunga mabao 17 katika michezo 33, likiwemo la bao la kwanza katika fainali ya Kombe la Ujerumani aliposhinda kombe kubwa la kwanza maishani mwake.
Baadaye alikiwasha kwenye michuano ya Euro ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 mwezi uliopita na kumaliza michuano hiyo akiwa mfungaji bora na mabao sita Ujerumani ilipotinga fainali, ambapo walifungwa 3-2 na Uingereza.
The post Newcastle yapata mrithi wa Isak first appeared on SpotiLEO.