Klabu Fenerbahce wameamua kumfuta kazi kocha wao Jose Mourinho. Klabu hiyo ya Uturuki imeamua kuachana na Mourinho ikiwa ni siku mbili baada ya klabu hiyo kuondolewa na Benfica katika mchujo wa Ligi ya Mabingwa.
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea, Manchester United, na Tottenham alijiunga na Fenerbahce msimu wa joto wa 2024, miezi sita baada ya kutimuliwa na Roma.
Aliiongoza timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita lakini akashindwa kupata taji lolote.
Fenerbahce ilifungwa 1-0 na Benfica katika mchezo wa mkondo wa pili wa mchujo wa kuwania kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.