DAR ES SALAAM: KAMPUNI ya Bolt Tanzania imemkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano la Bolt TZ Dance Challenge zawadi ya shilingi milioni 2.5 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mshindi huyo, Julius Bernard maarufu kama Juju Kida, aliibuka kidedea kutokana na umahiri wake wa kisanaa na ubunifu wa kitamaduni.
Awali, Juju Kida alishinda shilingi 300,000 katika shindano la ngoma lililoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri, na sasa amejinyakulia tuzo kubwa zaidi inayomtambulisha kama mmoja wa nyota wapya wa dansi nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya, Dimmy Kanyankole, alisema shindano hilo lilifanyika kuanzia Julai hadi Agosti 25 na lilijumuisha muziki, ngoma na tamaduni zilizowavutia mamia ya washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini.
“Shindano hili limeonesha ubunifu na ari ya vijana wa Kitanzania. Kampeni hii iliendeshwa kupitia wimbo wa asili uitwao Safari ni Bolt, uliotungwa mahsusi kuonesha mshikamano na safari za kila siku,” alisema Kanyankole.
The post Juju Kida alamba milioni 2 za Bolt dance challenge first appeared on SpotiLEO.