MGOMBEA Mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na Wananchi wa wilaya ya Busega,wakati alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya Msingi Mkula,Busega mkoani Simiyu kuanza mikutano ya Kampeni katika mkoa huo leo Jumatatu Septemba 1,2025.
Dk.Nchimbi alikuwa mkoa wa Mara na sasa ameingia mkoa wa Simiyu kuendelea na kampeni katika Mkoa huo,ambapo ameanza na jimbo la Busega.
Akiwahutubia wananchi wa Busega mkoani Simiyu, Balozi Dkt.Nchimbi alisema Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuuletea maendeleo zaidi mkoa wa Simiyu.
Pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Busega , Simon Songe sambamba na Wagombea Ubunge wengine pamoja na Madiwani wa Mkoa huo.