Marc Guehi ni rasmi atasalia Crystal Palace licha ya kufanyika kwa makubaliano ya kujiunga na klabu Liverpool mapema siku ya leo kabla ya Crystal Palace kubadilisha mawazo ya kumuachia baada ya kumkosa mbadala wake.
Beki huyo alikamilisha vipimo vya afya baada ya ada ya ofa kukubaliwa lakini dili hilo limekufa rasmi kufuatia kukosekana kwa mchezaji mwingine wa kuziba pengo lake baada ya Palace kumkosa Julio Igor.