Mchambuzi wa soka @mzeewajambia ameandika ujumbe kuhusu kauli ya Kocha Mkuu wa Simba aliyoisema hivi karibuni ya kumuhitaji mchezaji mwingine kwenye eneo lake la ushambuliaji.
“Juzi Fadlu Davids aliposema anahitaji xfactor Player mmoja ili Kikosi chake Kikamilike nafikiri hakueleweka Vizuri.
Manake watu walianza Kusema Mbona ana Neo Maema,Elie Mpanzu na Bajaber? Ahoua?
Lakini Fadlu anafahamu Vigezo vya sasa hivi ili uwe bingwa wa Ligi Kuu unahitaji Kuwa na Kikosi bora zaidi Kuliko Yanga Africa.
Yani Kikosi chako Kikiwa sawa na au chini ya Yanga Africa ujue huna chako hapo.
Kwasababu ni Ukweli Usiopingika Kwamba Kwenye Ligi Simba Sports anacheza Mechi nyingi ngumu Kuliko Yanga Africa”Ameandika @mzeewajambia .