DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’, amemuoa rasmi mwigizaji maarufu wa filamu za Bongo Movie, Chanuo, ambaye hapo awali alikuwa mke wa muigizaji Madebe.
Chanuo na Madebe walibahatika kupata watoto wawili kabla ya ndoa yao kuvunjika.
Chanuo anakuwa mke wa pili wa Tunda Man, jambo lililozua gumzo kubwa mitandaoni, hasa baada ya Chanuo kupakia picha za harusi kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amevalia mavazi ya harusi, akionekana mwenye furaha tele.
Picha hizo zimewaacha mashabiki midomo wazi, huku baadhi yao wakitoa maoni ya hisia mseto. Wapo wanaompongeza kwa kuanza maisha mapya, lakini pia wapo wanaomzodoa Madebe, wakidai huenda anaumia kwa kumuona ex wake akiolewa na mtu maarufu zaidi katika tasnia ya burudani.
The post Tunda Man aoa ‘Ex’ wa Madebe! first appeared on SpotiLEO.