Michuano ya kuwania kufuzu kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa ukanda wa Afrika inaendelea tena leo Septemba 05, 2025 ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itatupa karata yake nyingine kwenye mchezo wa Kundi E dhidi ya Congo Brazaville.
Baada ya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Alphonse Massamba-Debat mjini Brazzaville majira ya Saa moja kamili usiku (1:00) kwa Saa za Afrika mashariki, Stars itacheza tena mchezo mwingine wa kufuzu Kombe la Dunia Septemba 09 dhidi ya Niger katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
19:00 Congo π¨π¬ vs πΉπΏ Tanzania
22:00 Morocco π²π¦ vs π³πͺ Niger
MSIMAMO KUNDI E
1.π²π¦ Morocco β mechi 5 β pointi 15
2.πΉπΏ Tanzania β mechi 5 β pointi 9
3.πΏπ² Zambia β mechi 5 β pointi 6
4.π³πͺ Niger β mechi 4 β pointi 6
5. π¨π¬ Congo β mechi 5 β pointi 0
7. πͺπ· Eritrea β mechi 0 β pointi 0
NB: Eritrea ilijiondoa kwenye michuano hiyo kuepuka wachezaji kutumia fursa ya mechi za nje ya nchi na kutoroka Nchi hiyo kutokana utawala dhalimu wa Rais wa Nchi hiyo, Isaias Afwerki, ambao unalazimisha utumishi wa kijeshi wa maisha kwa watumishi
βΒ