RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametangaza hali ya hatari kwa waamuzi watakaochezesha ligi msimu ujao.
Akifunga semina ya waamuzi iliyokuwa ikifanyika makao makuu ya TFF, Karia amesema msimu ujao utakuwa tofauti ambapo watahakikisha wanasimamia umakini katika uchezeshaji.
Karia ambaye ameambatana na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Nassoro Idrissa amesema waamuzi ambao watashindwa kufanya uamuzi kwa ubora wataondolewa moja kwa moja kwenye majukumu hayo.