Klabu ya SIMBA SC imetangaza Mlinda mlango, Ally Salim hatakuwa sehemu ya kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili.
Ally alijiunga na Simba akiwa kijana mdogo katika msimu wa 2016/2017 akitokea timu ya Makorora FC ya Tanga ambapo alijiunga na timu ya vijana.