NEWYORK: MWANAMUZIKI nyota kutoka Marekani, Ciara Wilson ‘Ciara’, ametaja sababu ya kufanya wimbo wa ushirikiano na Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ni ule uwezo wake wa kucheza.
Wawili hao wamefanya wimbo wa pamoja unaoitwa Low ambao unapatikana katika albamu ya Ciara ya CiCi.
Katika mahojiano na BET, Ciara amesema Diamond ana uwezo mkubwa wa kucheza jambo linaloongeza mvuto katika video hiyo inayofanya vizuri kwa sasa.
Wimbo huo ukiwa na wiki mbili tangu uachiwe unashika nafasi ya pili kwenye mtandao wa Youtube ukiwa umefikisha watazamaji milioni 2.6.
Ciara aliongeza kuwa amevutiwa pia na nidhamu na utu wake akisema kuwa msanii huyo ana upekee unaoweza kumpeleka mbali zaidi kimataifa.
The post Ciara avutiwa uchezaji wa Diamond first appeared on SpotiLEO.