DAR ES SALAAM: STAA wa muziki na filamu nchini Tanzania, Lulu Abas maarufu kama Lulu Diva, ameweka wazi kuhusu sakata la kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa mwanamitindo Hamisa Mobetto, raia wa Nigeria Kelvin Sowax.
Akizungumza na Spoti leo, Lulu amethibitisha kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Kelvin, lakini akasisitiza kuwa walianza mahusiano yao baada ya Kelvin kuachana rasmi na Hamisa.
“Sio dhambi kuwa na uhusiano na mtu ambaye tayari ameachana na mpenzi wake. Watu wanaachana, maisha yanaendelea. Sidhani kama kuna kosa hapo,” amesema Lulu Diva.
Ameongeza kuwa madai ya kuachwa hotelini bila malipo ni ya uongo na hayana msingi wowote.
“Wanaosema niliachwa hotelini bila kulipiwa hawana wanachokijua. Wanaeneza tu maneno ya mitandaoni bila ukweli wowote,” amesisitiza.
The post Lulu Diva azungumzia penzi la ‘ex’ wa Mobetto first appeared on SpotiLEO.