LIVERPOOL: MENEJA wa Liverpool Arne Slot amewataka Mashabiki wa klabu hiyo waliojaa hamu ya kumuona mchezaji wao mpya aliyesajiliwa kwa rekodi ya Premier League Alexander Isak akicheza kwa mara ya kwanza wikiendi hii kuwa watulivu wakati huu Msweeden huyo akiingia kikosini taratibu.
Isak alikamilisha usajili wa pauni milioni 125 kutoka Newcastle United hadi kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England katika siku ya mwisho ya usajili, na hivyo kuhitimisha sakata la uhamisho wake lililokuwa likiendelea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amecheza kwa dakika 18 pekee msimu huu, nazo ni katika michezo ya kufuzu kombe la Dunia akitokea benchi taifa lake likipokea kipigo cha 2-0 kutoka kwa Kosovo Jumatatu.
Slot amemsifu kocha wa Sweden Jon Dahl Tomasson kwa kumtumia Isak kwa uangalifu na akasema Liverpool pia itampa dakika kidogo ili aweze kufit kwenye mipango yake msimu huu.
“Tutampa Alex dakika sawa nae (kocha wa Sweden). Msitarajie kuwa kila mechi atacheza dakika 90. Hilo halitafanyika katika hivi karibuni. Hakuwa na maandalizi mazuri ya msimu, amekosa mazoezi kwa miezi mitatu au minne” – Slot aliwaambia wanahabari kabla ya mechi ya Jumapili.
“Lazima tumjenge hatua kwa hatua, hatujamsajili atutumikie kwa wiki mbili zijazo, tumemsajili kwa miaka sita, kwa hivyo hili ndilo tunalopaswa kukumbuka na ambalo mashabiki wanapaswa kuzingatia.” Aliongeza
Liverpool wako kileleni mwa EPL na pointi tisa walizovuna kwenye michezo mitatu ya Ligi hadi sasa. Jumapili watakuwa wageni wa Burnley katika dimba la Turf Moor
The post Slot awapoza mashabiki kwa Isak first appeared on SpotiLEO.