NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE mteule wa viti maalum Vijana Taifa kwa tiketi ya CCM kutoka mkoa wa Iringa, Jasmine Ng’umbi amejitokeza katika majukwaa kumnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na wagombea ubunge na madiwani wa Ccm mkoa Iringa kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Kalenga na Iringa Mjini, Jasmine Ng’umbi alisema kuwa kwa mambo mbalimbali na miradi ya maendeleo aliyofanya mgombea wa CCM Mama Samia anastahili kurudi tena kuongoza nchi yetu.
Alisema kuwa kura zote zitakwenda kwa CCM kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani, wakiamini katika dira ya maendeleo ya chama hicho ya mwaka 2025-2030 ambapo imevipaumbele vinavyomgusa mwananchi wa chini kabisa.
Aliongeza wananchi wanatakiwa kusimama imara na kuhakikisha wanachagua viongozi wa CCM kwani ndio wenye uwezo wa kweli katika kuleta maendeleo .
Alisema kuwa katika sekta mbalimbali CCM iliahidi na kutekeleza shule ziko nyingi, maji yapo ya kutosha, hospitali zimejengwa, vituo vya afya Rais amefanya mambo makubwa ya maendeleo,” alisema
Jasmine alisema kuwa kazi ya kusema ni ya mwanaume na kazi ya kutenda ni wanawake, akina mama ni waaminifu wa hiyo Rais Samia amefanya kazi nzuri lakini na Chama Cha Mapinduzi kinafanya mengi mazuri zaidi hivyo wananchi wanatakiwa kukipa kura za kutosha.