MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewahutubia Wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa, leo Jumamosi Septemba 13,2025 mkoani Kilimanjaro.
Baada ya kupokewa na kuwahutubia Wananchi uwanjani hapo,Dkt
Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini Ndugu Ibrahim Mohamed Shayo pamoja na Madiwani.
Dkt.Nchimbi ambae ameingia Kanda ya Kaskazini,akianzia mikutano yake ya Kampeni Mkoani Arusha na sasa anaendelea mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.