

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani WHO, kuna ongezeko kubwa la unene kupindukia miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 19.
Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya tatizo la watu kunenepa kupindukia ambalo limeongezeka maradufu miongoni mwa watoto na vijana. Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema matumizi ya vyakula vinavyotengenezwa viwandani na matangazo ya vyakula visivyofaa kiafya yamelifanya tatizo hilo kuongezeka mno.
UNICEF imeonya kwamba kwa sasa tatizo hilo limeongezeka zaidi miongoni mwa watoto wa umri wa miaka mitano hadi vijana wa miaka 19 na kwa sasa limepita hata tatizo la utapiamlo.
Ripoti ya UNICEF imefafanua kwamba kama ambavyo ilitarajiwa awali kwamba hadi mwisho wa mwaka huu wa 2025 mtu mmoja katika kundi hilo la la watu atakuwa na tatizo la kunenepa kupita kiasi.
Mkuu wa shirika la UNICEF Catherin Rusell amesema kwamba maana ya neno utapiamlo sasa linabadilika kutokana na tatizo hilo.
“Leo tunapozungumzia utapiamlo hatumaanishi ukosefu wa lishe bora wala kukonda kupita kiasi.”
Katika ripoti yenye kutia wasiwasi kutoka shirika la UNICEF vyakula vya viwandani vinaendelea kuchukua nafasi ya matumizi ya matunda,mboga na protini katika kipindi ambacho mtoto anahitaji aina hii ya vyakula katika makuzi yake.
Shirika hilo linasema kwamba jambo la kutisha ni kwamba kwa hali hii mtu 1 kati ya 10 walioko kwenye kundi hilo la umri wa miaka 5 hadi 19 anakabiliwa na magonjwa sugu yanayosababishwa na urahisi wa kupata vyakula hivi vya viwandani.
Katika hali ambayo haikutegemewa kiasi cha watu wenye tatizo la unene wa kupindukia kwa mara ya kwanza limepanda kwa asilimia 9.4% zaidi ya watu wenye tatizo la kukonda kupita kiasi chini ya kiwango katika asilimia 9,2%.
Kulingana na makadirio ya ripoti ya UNICEF watu milioni 188 wakiwemo watoto na vijana kote ulimweguni wana tatizo la uzito wa kupindukia kutokana na kula vyakula vyenye wanga, sukari na kutojali ulaji sahihi. Wananchi wametakiwa kuepuka vyakula hivyo.
STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL
”NAPENDA UIGIZAJI WA ELIUD – MBONA HUJANIALIKA DADA’AKO KWENYE HARUSI” – MATUMAINI WA KIWEWE…