Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemtangaza mwamuzi Ahmed Arajiga, kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakao wakutanisha Yanga na Simba kwenye uwanja wa Mkapa.
Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo, amesema Arajiga atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo, akisaidiwa na Mohammed Mkono, atakayekuwa mwamuzi msaidizi wa kwanza na Kassim Mpanga, atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.
Aidha Ndimbo amesema, mwamuzi wa nne atakuwa Ramadhan Kayoko.
Rekodi zinaonyesha hii itakuwa ni Dabi ya tano kwa mwamuzi Arajiga, kutoka Babati kuamua mchezo huo.
Yanga ndio wenye bahati na Arajiga, ambapo kwenye mechi nne zilizoamuliwa na mwamuzi huyo, imeshinda tatu na kupoteza moja