YANGA SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz imetwaa taji la Ngao ya Jamii kwa ushindi mbele ya watani zao wa jadi Simba SC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Bao pekee la ushindi kwa Yanga SC limefungwa na Pacome dakika ya 53 akiwa ndani ya 18 akimfunga kipa Moussa Camara ambaye alianza kikosi cha kwanza.
Yanga SC wameanza msimu wa 2025/26 wakitwaa taji ambalo walikuwa wanalitetea baada ya kutwaa msimu wa 2024/25 mbele ya Azam FC.
Simba SC haijawa na bahati mbele ya Yanga SC kwa kuwa msimu wa 2024/25 katika mechi tatu walizokutana uwanjani walikwama kupata ushindi.
Kwa mara nyingine tena Yanga SC wameendeleza ubabe wao kwa kupata ushindi ikiwa ni mara ya nne mfululizo mbele ya Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Kibu Dennis na Ellie Mpanzu ambao walianza kikosi cha kwanza nafasi ambazo walizitengeneza katika kipindi cha kwanza walikwama kuzibadili kuwa mabao jambo ambalo liliwapa tabu mpaka mwisho wa mchezo.