Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Ashura Katunzi akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari kuhusiana ma mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita.
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) katika mafanikio ya Serikali ya Sita wamesogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga maabara za Kisasa katika katika Mikoa ya Dodoma pamoja na Mwanza.
Ujenzi wa Maabara kwa Mkoa Dodoma kwa ajili ya kuhudumia Kanda ya Kati kwa Mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora pamoja na Kigoma na Ofisi ya Mwanza kuhudumia Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza ,Kagera ,Shinyanga,Mara ,Simiyu pamoja na Geita.
Akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katika Mikutano inayoratobiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Ashura Katunzi amesema Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu na kupunguza gharama, Serikali kupitia TBS limeanza ujenzi wa maabara katika mikoa ya kimkakati ya Dodoma na Mwanza utaogharimu zaidi sh.Bilioni 36 na Dodoma unagharimu zaidi ya sh.Bilioni 12
Amesema sehemu ya jitihada za Serikali katika kuimarisha miundombinu ya sekta za Viwanda na Biashara ili kukuza uchumi wa Taifa .
Aidha amesema Mafanikio hayo yameendelea kutimiza azma ya Shirika katika masuala mbalimbali ili kutimiza matamanio ya wadau na Taifa kwa kwa kusogeza huduma Karibu na Wateja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli.
Dkt.Amesema Serikali kupitia TBS imetumia zaidi ya TZS 9.8 bilioni kwa ajili ya kuimarisha ofisi tisa za kanda (Arusha, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma, Mbeya, Pwani na Geita) pamoja na ofisi za mipakani (Tunduma, Kasumulo, Horohoro, Holili, Tarakea, Namanga, Bandari ya Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Sirari, Kabanga, Rusumo, Mutukula, Kasesya, Bandari ya Bagamoyo, bandari ya Mbweni, bandari ya Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere – Dar es Salaam na Bandari ya Tanga) kwa kuongeza ofisi mpya za kanda, wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara katika soko ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na hatimaye kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama.
Hata huvyo amesema katika Kuwezesha Biashara TBS imekuwa na Kamati za Kitaalam ,Uandaaji Viwango 115 katika sekta ya chakula, kemikali, uhandisi mitambo, uhandisi umeme, uhandisi ujenzi, nguo na ngozi, madini na mitambo ya uchimbaji madini, mazingira na katika mchakato wa kuandaa viwango Kamati hizo zinashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wafanyabiashara, wazalishaji, vyama vya walaji, vyama na bodi za wataalam, taasisi za udhibiti na watunga sera.
Amesema katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita Shirika limefanikiwa kuandaa viwango 2,765 vya sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya soko ambavyo vitasaidia wafanyabiashara, wajasiriamali na watoa huduma kuzalisha bidhaa bora zenye kukidhi matakwa ya viwango, hivyo kuwawezesha kufanya biashara ndani na nje ya nchi, hatua ambayo italeta tija na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Aidha, jumla ya vyeti na leseni za ubora 3,184 vimetolewa kwa wazalishaji, miongoni mwao wakiwemo wajasiriamali wadogo 1,359. Serikali kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya TZS milioni 350 kila mwaka kwa madhumuni ya kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote. Leseni hizi zimesaidia wazalishaji kuweza kuzalisha bidhaa bora, ikiwa ni pamoja na bidhaa zao kuweza kuaminika sokoni na pia kufanya biashara nje ya mipaka ya Tanzania, hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Mkurugenzi Mkuu amesema shirika limeendelea na huduma za usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi pamoja na maeneo ya uzalishaji, uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa chakula na vipodozi kwa lengo la kuhakiki ubora na usalama wa maeneo hayo ili kuendelea kulinda afya za walaji ambapo jumla ya bidhaa 8,199 zilisajiliwa na maeneo 47,886 yalisajiliwa.
Pia, katika kuimarisha ukaguzi wa bidhaa mbalimbali zinazoingia nchini kutoka nchi za nje, TBS huhakiki ubora wa bidhaa na magari yaliyotumika kabla ya kusafirishwa kuja nchini.
Dkt.Katunzi amesema katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita jumla ya shehena za bidhaa 153,159 zilikaguliwa kabla ya kuingia nchini kupitia mfumo na shehena za bidhaa 352,103 zilikaguliwa baada ya kufika nchini kupitia mfumo.
Amesema magari 203,689 yalikaguliwa kwa lengo la kuiepusha Tanzania kuwa jalala la bidhaa duni.
Amesema katika kujiimarisha TBS imetoa mafunzo kwa jumla ya wadau 5,437 wakiwemo wazalishaji wa bidhaa za viwandani na wasindikaji yaliyohusu dhana nzima ya viwango na ubora ambayo yatawawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango na yamewawezesha kupata uelewa mpana kwenye masuala ya udhibiti ubora, hivyo kuwaandaa kuhimili ushindani wa masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.
Amesema kupitia Mradi wa Qualitan TBS na SIDO mwaka 2024 waliwezeshwa kutoa mafunzo kwa wazalishaji wa bidhaa za chakula 1000 katika mikoa 10 (Dar es Salaam, Singida, Mwanza, Geita, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Tanga, Ruvuma na Kilimanjaro)
Vilevile, TBS imeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ili kukuza uelewa juu ya masuala ya viwango na udhibiti ubora.
Amesema katika kuongeza Ufanisi wa Maabara TBS ina jumla ya maabara 12 na zote zimeweza kupata ithibati za umahiri, ambapo maabara hizo zimehakikiwa na kupatiwa vyeti vya ithibati ya umahiri wa kimataifa.
Dkt.Katunzi TBS imeweza kupima sampuli zaidi ya 152,812 na kufanyia ugezi vifaa 42,993 ambapo suala hili litasaidia kuhakikisha katika soko kunakuwa na bidhaa zenye ubora kuongeza kuwa Maabara za TBS zina mashine za kisasa zinazopelekea kupata majibu kwa wakati na sahihi, Serikali imeweza kutumia kiasi kisichopungua TZS 12.9 bilioni kuhakikisha mashine hizi zinapatikana.
Amesema pamoja na mashine nyingi zilizopo katika maabara hizo, kuna mashine za kipekee ambazo ni Mashine ya hydrostatic pressure test ya kupima mabomba ya maji na yenye uwezo wa kupima mabomba yenye kipenyo cha milimita 12 sawa na inch 0.5 hadi milimita 800 sawa na inchi 32. Mashine hii ina uwezo pia wa kupima sampuli 120 kwa wakati mmoja na kati ya nchi 54 za Barani Afrika inapatikana katika nchi tano tu ikiwemo Tanzania.
iMashine zingine ni zile ya automatic conductor resistance tester ya kupimia waya (cables) za umeme za aina zote zenye kipenyo hadi kufikia milimita 40 sawa na milimita za mraba1200 pamoja na mashine hii ni ya kipekee kwa kuwa ni ya kidigitali na ina uwezo wa kupima na kutoa majibu kwa haraka ,Mashine ya solar simulator ambayo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inapatikana Tanzania pekee katika ofisi zetu za TBS. Mashine hii inauwezo wa kupima solar panels za aina zote bila kutegemea uwepo wa jua.
Shirika linatumia mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kama vile leseni ya ubora, ukaguzi wa shehena zinazotoka nje ya nchi na usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi, majengo, maeneo ya uzalishaji, uuzaji, vyombo vya usambazaji wa bidhaa za chakula na vipodozi. Mifumo hiyo ni OAS na i-SQMT. Aidha, Shirika limeboresha huduma zake kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini kwa kuunganisha mfumo wake unaoitwa Online Application System na mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Tanzania electronic Single Window System – TeSWS) ambapo mfanyabiashara anatuma maombi na anapata huduma za taasisi zote na kibali kupitia mfumo huo.
Amesema katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Serikali katika kuboresha upatikanaji wa nishati safi, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, na kutunza mazingira huku ikiokoa maisha kupitia suluhisho endelevu la upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kupitia TBS na washirika wa maendeleo na Wizara ya Nishati imeanza kuandaa viwango vya ufanisi wa nishati kwa vifaa vya umeme vya majumbani.
Shirika hilo limeweza kupata Tuzo na Umahiri
Mnamo mwaka 2023, TBS ilipata mafanikio kwa kushinda Tuzo ya kuwa Mdhibiti Bora Barani Afrika kwa Mwaka 2023 inaonesha dhamira ya TBS katika utendaji bora na mchango wake chanya katika kukuza viwango na kudhibiti ubora.?
Amesema TBS imekuwa taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kupata ithibati (accreditation) ya mifumo ya udhibiti ubora wa bidhaa (Product Certification) ya kimataifa katika wigo mpana (wide scope) ndani ya muda mfupi na ni ya taasisi ya tatu kupata ithibati hiyo iliyotolewa na SADCAS Septemba, 2024 hivyo kufanya mifumo hiyo kutambulika kimataifa.
Pia kwa mwaka 2025, TBS imefanikiwa kupata ithibati ya umahiri wa mfumo wa usimamizi wa chakula katika kiwango cha kimataifa toleo jipya (ISO 22003:2022). Kuhamia kwenye ithibati hii kunaifanya TBS kuwa taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kupiga hatua hiyo. Ithibati hii ni ishara kuwa TBS inafanya kazi zake kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa iliyowekwa na hivyo kuendelea kuaminiwa na wateja na wadau wengine TBS pia tunajivinua kuwa na wataalam wenye umahiri na weledi mpaka kutambulika kimataifa, kwani wataalam wa TBS hualikwa na SADCAS kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalam katika masuala ya ithibati (accreditation) kwenye maeneo ya Metrolojia (metrology), uthibitishaji wa ubora (certification), na ukaguzi (inspection) kwa taasisi na mashirika yanayohitaji huduma hizo katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Shirika kupitia wataalam wake liliweza kutoa Mshindi wa ISO Next Generation Award kwa mwaka 2023, Tuzo iliyoandaliwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) ambayo ilikuwa na lengo la kutambua mchango wa wataalam katika kuandaa viwango vinavyochagiza maendeleo endelevu ya kimataifa (UN SDGs).Shindano hili lilihusisha maafisa viwango wenye umri chini ya miaka 35 kutoka nchi takribani 175 wanachama wa ISO na mtaalam kutoka TBS aliibuka mshindi na kukabidhiwa tuzo husika huko Brisbane,Australia.
Serikali kupitia TBS inaendelea na juhudi za kuweka na kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuboresha huduma kwa lengo la kuwezesha biashara kwa madhumuni ya kuinua uchumi wa viwanda kwa kuchagiza uzalishaji wa bidhaa salama na bora hapa nchini kama njia mojawapo ya kuchangia pato la Taifa.