MANCHESTER: MSHAMBULIAJI wa Manchester City Erling Haaland amekuwa mchezaji aliyetumia mechi chache zaidi kufikisha mabao 50 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Napoli usiku kuamkia leo.
Haaland iliivuka rekodi ya awali ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid Ruud van Nistelrooy, ambaye alitumia mechi 62 kufikia jumla hiyo, katika mchezo wake wa 49 katika mashindano hayo makubwa ya soka ya kwa ngazi Klabu barani Ulaya.
“Inaonekana atavunja kila rekodi iliyopo. Katika umri aliopo, anachokifanya hakielezeki kwa maneno ya kawaida,” – mchezaji mwenzake Phil Foden alisema.
Akiwa na umri wa miaka 25, Haaland anaonekana kuwa na uwezo wa kufukuzia rekodi ya muda wote ya Cristiano Ronaldo kwenye Ligi ya Mabingwa ya mabao 141.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema anaamini ikiwa Haaland atacheza kwa zaidi ya miaka 10, 12 kwa kiwango sawa na cha sasa anaweza kufikia rekodi hiyo.
Awali, Haaland aliipiku rekodi kama hiyo ya Van Nistelrooy ya kufunga mabao 30 kwenye Champions League, mwaka 2023. Mwaka huohuo akawa mchezaji aliyetumia mechi chache zaidi kufunga mabao 50 kwenye Premier League.
Hadi sasa, ana jumla ya mabao 130 katika mechi 151 tangu ajiunge na Manchester City akitokea Borussia Dortmund mwaka 2022.
The post Haaland aweka rekodi nyingine UCL first appeared on SpotiLEO.