MAKALA: WALIOPO karibu na na staa wa Yanga, Celestin Ecua wamwambie ukweli kuwa tayari ameshafika jijini Dar es Salaam na yupo na jezi ya timu yenye mataji mengi zaidi nchini Yanga.
Kisha wamwambie kuwa Yanga wanakusifia leo na kesho wanakukataa wanachojali wao ni furaha yao tu mengine hayawahusu.
Lakini msisahau kumwaambia kuwa wanazi wa Simba na Yanga kutwaa wao ni kuzungumza kuhusu timu zao, yaani ni kama dozi kutwa mara tatu.
Mkumbusheni kuwa linapokuja suala la timu hizi wanazoziita za urithi kutoka kwa mababu zao kuna muda wapo tayari hata kujitoa akili ili tu kupigania nembo ya timu yao iwe kwa maneno au kwa vitendo.
Kwa michezo michache aliyoonekana akiwa na uzi wa Yanga, Ecua ameonekana kuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini mwenye mambo mengi uwanjani.
Kwenye mchezo dhidi ya Simba, alipata nafasi ambayo alipaswa kufanya maamuzi bora zaidi lakini aliishia kuukokota mpira na kupoteza nafasi ya dhahabu ambayo ingeumaliza mchezo.
Mashabiki wa Yanga hawajalisahau tukio hilo ila wameamua kufurahia kwanza ushindi dhidi ya mtani na kisha huenda watamrejea tena ikiwa tukio hilo litajirudia kwani hata kwenye mchezo dhidi ya Rayon Sports na Bandari kulikuwa na matukio ya aina hiyo.
Bado mapema akumbushwe kuwa ni rasmi yupo kwenye nchi ambayo mashabiki watamba kuujua mpira kuliko wataalamu na uvumilivu ndo kitu kilichowashinda tangu zama za kale.
The post Ecua akiwahiwa anapona, kazi kwake! first appeared on SpotiLEO.