NA DENIS MLOWE, IRINGA
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Iringa Mjini, Frank Nyalusi amefariki dunia usiku wa kumkia leo katika Hospital ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
Nyalusi aliyekuwa akiumwa kwa kipindi cha miezi kadhaa taarifa yake imetolewa mapema asubuhi ya leo na familia yake ikisema kwamba ‘Kwa masikitiko makubwa tunapenda kutoa taarifa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa M/Kiti Frank John Nyalusi kwamba amefariki usiku wa leo.
Mwenyezi Mungu akampe pumziko la Milele. Akawe mfariji kwa familia, Ndugu, jamaa na marafiki na wanachama wote wa CHADEMA. Tunamshukuru Mungu kwa maisha yake hapa duniani
Nyuma yetu mbele yake Hakika Vita umevipiga na mwendo umeumaliza tutaonana baadae kaka wa wote”
Katika hali ya huzuni zaidi kwa familia ya Nyalusi wiki mbili zilizopita Nyalusi alifiwa na mama yake mzazi ghafla mara baada ya kumwona kijana wake akiwa katika hali mbaya ya kuumwa alipokuwa amelazwa katika Hospital ya Wenda.