DAR ES SALAAM: MREMBO kutoka kiwanda cha muziki wa kizazi kipya, Irene Louis ‘Lynn’, amesema bado hajapoteza mvuto wake wa kimuziki, bali ameamua kujipa mapumziko kwa muda kabla ya kurudi kwa kishindo.
“Sidhani kama nimeharibika au kupoteza muonekano wangu wa awali. Mimi bado mzuri na soko langu lipo pale pale. Muziki ndiyo kila kitu hapa mjini, nimejipa muda ili niweze kulisoma game vizuri,” amesema Lynn.
Ikumbukwe Lynn aliwahi kuwa miongoni mwa wanawake waliomvutia mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ambaye aliwahi kutangaza kuwa yuko tayari kutoa mahari yoyote ili kufunga naye ndoa.
The post Lynn: Sijachuja, nimepumzika tu kimuziki first appeared on SpotiLEO.