Anaandika @kelvinrabson_
✍️ Yanga walianza mchezo vizuri sana wakati wanaanza build up wanakuwa na muundo wa 3-2 dhumuni ni kuishinda pressing ya Waliete ambayo walipress na muundo wa 4-1-4-1 lakini bado hawakufanikiwa kwenye mipango yao ….. How ?
1: Yanga hawakuitaji ufanisi mkubwa wa pasi zao kuishinda pressing ya Waliete kwasababu walipata nafasi kwenye mpira , positioning yao ilikuwa nzuri na ilitoa msingi mzuri wa kufika kwenye eneo la mbele kirahisi .
2: Walichokikosa Yanga ni matumizi ya nafasi ( Ufanisi mbele ya goli ) walitengeneza nafasi nyingi nzuri : Nafikiri walistahili kuimaliza game kipindi cha kwanza .
3: Yanga wasipokuwa na mpira walipress vizuri kuanzia juu ( Presha kwenye mpira na kwa mchezaji , walifika kwenye matukio kwa wakati sahihi + walishinda mipambano yao vizuri sana ni vile Yanga hawakuwa wakatili kwenye matumizi yao ya nafasi .
✍️ Kipindi cha Pili , Nafikiri Waliete waliboresha pasi zao wakati wanaanza build up : utulivu wakiwa na mpira , runners eneo la mbele + wakaanza kufika eneo la mbele tofauti na kipindi cha kwanza ….. nimependa actions aliyoichukua Roman Folz baada ya hapo Kwanini ?
✍️ Kwasababu Waliete wali risk kuifanya block kuwa juu zaidi , Yanga walihitaji wachezaji wengi wanao hitaji mpira kwenye nafasi na sio mguuni ( Runners ) wakiwa na mpira Edmund na Ecua wanakuwa pembeni kabisa ya kiwanja dhumuni ni kuwafanya FBs wa Waliete kuzuia eneo kubwa na kuacha nafasi eneo la ndani na walifanikiwa ( Msingi wa magoli mawili ya mwisho : Counter Pressing then positioning ya Edmund ilikuwa nzuri + runs ya Dube kwenye goli la tatu )
NOTE :
1: Aziz Andambwile kafanya kazi nzuri sana kwenye kiungo ( usahihi wa pasi zake , Positioning yake akiwa na mpira ✅ )
2: Dube kirahisi leo angeondoka na Hattrick .
3: Israel Mwenda kacheza game bora sana 🙌
4: Kuingia kwa Maxi Nzegeli kulileta uhai kwa Yanga wakati wanashambulia ( Uharaka kwa maamuzi , runs mzuri + positioning yake ilikuwa bora )
5: Edmund John game nzuri kwake 👍
FT : Wiliete 0-3 Yanga Sc