SEPTEMBA 20 2025 ni Gaborone United vs Simba SC mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wababe hawa watakuwa katika dakika 90 za kusaka ushindi kabla ya mchezo wa pili utakaotoa mshindi wa jumla atakayekwenda hatua inayofuata.
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wanachohitaji ni ushindi ili kutimiza malengo ya kwenda hatua ya makundi.
“Ili upate nafasi ya kwenda hatua ya makundi ambacho kinahitajika ni ushindi. Mechi zote iwe ugenini na nyumbani ni muhimu kushinda na sisi tumejiandaa kufanya hivyo.
“Timu yangu imecheza mechi mbili zenye uzito mkubwa Simba Day na Ngao ya Jamii kwa hiyo imetuongezea ubora.
“Hata hivyo namuheshimu sana kocha wa timu pinzani naiheshimu hii timu kwa sababu wao ni mabingwa,”.
Simba SC itakuwa Uwanja wa Francistown ikiwa ni hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Miongoni mwa wachezaji waliopo Botswana ni Ellie Mpanzu, Mousa Camara, Kibu Dennis, Joshua Mutale na Wilson Nangu. Miongoni mwa wachezaji ambao wataukosa mchezo wa leo ni Hamza ambaye ni beki alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC na Mohamed ambaye huyu alisajiliwa akiwa na majeraha bado hajawa imara.