Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Chrstopher Ngubiagai, akizungumza katika hafla ya kuanza kwa safari za kibiashara za Mel ya MV Butiama, leo katika Bandari ya Nansio.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Umma wa TASHICO, Anselem Namala, leo, akizungumza na wananchi wa Ukerewe, muda mfupi baada ya Meli ya MV Butiama, kuwasili Bandari ya Nansio, Ukerewe, kutoka Bandari ya Mwanza Kaskazini, kuanza safari za kibiashara .
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla ya mapokezi ya Meli ya MV Butiama, leo katika Bandari ya Nansio, Ukerewe.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ukerewe, Ally Mambile, leo akitoa salama za Chama katika mapokezi ya Meli ya MV Butiama ilipoanza safari za kibiashara tangu ilipositisha huduma Disemba 2024, kupisha matengenezo ya uwiano.
Nahodha wa MV Butiama, Silvanus Matiko (kushoto), akihojiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, kuhusu ufanisi wa meli hiyo, leo.
Baadhi ya wananchi wakwa ndani ya MV Butiama tayari kwa safari.
……..
NA MASHAKA, NANSIO, UKEREWE
Baadhi ya wananchi waliojitokeza leo, katika mapokezi ya Meli ya MV Butiama, katika Bandari ya Nansio, Ukerewe , kuanza safari za kibiashara. (Picha zote na Baltazar Mashaka)
……………..
MELI ya MV Butiama inayomilikiwa na Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) imeanza tena safari zake za kibiashara kati ya Bandari ya Mwanza Kaskazini na Nansio, Ukerewe, baada ya kusimama kwa miezi tisa kupisha matengenezo. Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Umma wa TASHICO, Anselem Namala, amesema matengenezo hayo yalifanywa baada ya kubainika meli hiyo kuwa na changamoto ya uwiano wa kuelea tangu Desemba 2024, na sasa imehakikishiwa usalama kwa abiria na mizigo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa safari hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, alisema kurejea kwa MV Butiama ni ushahidi wa utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na kwamba hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha miundombinu ya usafiri ndani ya Ziwa Victoria.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe, Ally Mambile, alimshukuru Rais Samia kwa juhudi za kuhakikisha wananchi wa Ukerewe wanapata huduma muhimu, akieleza kuwa kurejea kwa meli hiyo kumeongeza matumaini ya kiuchumi kwa wakazi wa kisiwa hicho.
MV Butiama imekuwa tegemeo muhimu kwa wakazi wa Ukerewe, ikihusisha usafirishaji wa abiria na mizigo. Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wameipokea kwa furaha meli hiyo, huku wakiomba kuongezewa idadi ya safari ili kuongeza ufanisi wa huduma.