Baada ya kuachana na vigogo wa Tanzania Simba SC, Kocha Fadlu Davids anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu ya Raja Club Athletic.
Makubaliano yote tayari yamekamilika na Fadlu anarudi katika klabu hiyo aliyowahi kuwa kocha msaidizi na kushinda Botola Pro bila kupoteza mchezo msimu mzima.
Kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini na kesho atasafiri kuelekea Morocco kuanza ukurasa mpya kama kocha mkuu wa Raja.
Vigogo hao wa Morocco wanataka kurejea kileleni, hasa katika mashindano ya kimataifa ya CAF, na wamemhakikishia Fadlu na benchi lake la ufundi sapoti ya kutosha kufanikisha mafanikio.