Baada ya mashabiki kumlaumu kocha CR Belouizdad ya Algeria, Sead Ramovic kwa kuamua kusafiri na kwenda nchini Hispania kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Real Madrid na Olympique Marseille badala ya kuwekeza nguvu kwa klabu yake iliyotoka kupoteza mchezo wa Ligi nyumbani dhidi ya Js Kabylie Septemba 13 huku ikitegemewa kuwa na mechi nyingine siku nne zijazo, Ramovic aliwajibu mashabiki hao na kusema maamuzi yake ya kwenda Hispania, Septemba 16 kunako jiji la Madrid haikuwa kwa ajili ya kuponda raha na kuwakosea heshima mashabiki.
Badala yake alilenga kwenda kutazama vema mbinu za kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso na zile za kocha wa Marseille, Roberto De Zerbi ili azitumie kuboresha timu yake….
Fastfoward!! Baada ya kurejea na hizo mbinu zake, ”Mzee wa Intensity” amelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya pili kutoka mkiani , Mc El Bayadh…
Kwa kifupi ni kuwa mbinu za Marseille na Real Madrid lilizozifuata ‘Zee la Intensity’ hazijasaidia kitu.