
Dar es Salaam: Moto mkubwa umezuka leo katika jengo lililopo pembe ya mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda wamesema moto huo ulianza ghafla na kuendelea kusambaa kwa kasi, huku chanzo chake kikiwa bado hakijafahamika. Vikosi vya zimamoto na uokoaji tayari vimefika eneo la tukio na kuendelea na juhudi za kuuzima.
Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo ikiwemo hasara za mali au majeruhi. Polisi na maafisa wa zimamoto wameeleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.