Baada ya kuripotiwa kwa taarifa kwamba kocha mkuu wa Simba SC, Fadlu David’s raia wa Afrika Kusini kutaka kuondoka kwenye kikosi hicho na ikielezwa kuwa tayari Waarabu wametenga dau la kumng’ oa Msimhazi, inasemekana warithi wake wanatajwa ambao ni Miguel Angel Gamondi wa Singida Black Stars na Benn McCarthy wa Harambee Stars.
Chanzo changu cha habari bila shaka akijaficha kitu, kimesema wazi kwamba tajiri wa Simba SC, Mohamed Dewji au maarufu MO Dewji kama asipofanikiwa kumbakisha Fadlu, anamshusha kocha wa Singida Black Stars Miguel Angel Gamondi ambaye pia aliwahi kuifundisha Yanga, pia endapo Gamondi akikosekana basi atamleta kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Benn McCarthy raia wa Afrika Kusini.