Raja Club Athletic wamemtambulisha aliyewahi kuwa kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, kama kocha wao mkuu mpya. ✍️
🟢 Katika taarifa yao rasmi, Raja walisema:
“Davids alikuwa miongoni mwa watu muhimu katika historia ya msimu wa 2023/24, ambapo tulitwaa ubingwa wa Botola Pro bila kufungwa.” 👑
Kocha huyu mwenye falsafa ya soka la kisasa anaingia Morocco akiwa na kumbukumbu nzuri za mafanikio, huku mashabiki wa Raja wakitarajia mwendelezo wa ubora na historia mpya chini yake.