Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans Sc, Fiston Kalala Mayele amefunga magoli matatu wakati, Pyramids Fc ikiiondoa Al Ahli Saudi ya Saudi Arabia kwa jumla ya mabao 3-1 katika Kombe la Mabara la FIFA 2025.
Al Ahli Saudi imeondoshwa kwenye michuano hiyo licha kusheheni baadhi ya majina makubwa wakiwemo winga wa zamani wa Man City, Riyad Mahrez, kiungo wa zamani wa Barcelona, Franck Kessie na mshambuliaji wa zamani wa Brentford, Ivan Toney aliyefungia bao pekee la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati.
Pyramid watamenyana na Mabingwa wa Amerika Kaskazini/Kusini na Mshindi atakutana na PSG katika fainali. Klabu hiyo itakuwa nchini Rwanda wiki ijayo kumenyana na APR FC katika Mashindano ya klabu bingwa Afrika.
FT: Al Ahli Sc πΈπ¦ 1-3 πͺπ¬ Pyramids
β½ 45β Toney (P)
β½ 21β Mayele
β½ 71β Mayele
β½ 75β Mayele
βΒ