Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefika katika mradi wa maji wa Butimba kufuatilia marekebisho yanayoendelea ili kurejesha huduma ya maji katika hali ya kawaida kutokana na hitilafu iliyotokea katika mtambo wa kusukuma maji.
Mhandisi Mwajuma amefanya kazi kwa saa 24 na wataalam katika kurekebisha hitilafu iliyojitokeza kwa lengo la kuhakikisha maji yanapatikana kwa wananchi muda wote kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali katika mradi wa maji wa Butimba.